Nguvu ya Kuwa na Nia Chanya

Nguvu ya Kuwa na Nia Chanya

Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. —Mithali 23:7

Miaka mingi iliyopita, nilikuwa mwenye nia hasi kabisa. Filosofia yangu yote ilikuwa hii: “Usipotarajia kitu chochote kizuri kufanyika, basi hutasikitika kisipofanyika.” Kwa hivyo vitu vingi viharibifu vikanifanyikia kwa muda wa miaka mingi, niliogopa kuamini kwamba kitu chochote kizuri kinaweza kunifanyikia. Kwa kuwa nia yangu ilikuwa hasi yote, hivyo pia mdomo wangu ukawa; na pia maisha yangu.

Pengine uko vile nilivyokuwa. Unajiepusha na tumaini ili kujikinga kutokana na kudhurika. Aina hii ya tabia huanzisha mtindo hasi wa maisha. Kila kitu kinakuwa hasi kwa sababu mawazo yako ni hasi.

Kwa kweli nilipoanza kusoma Neno la Mungu na kuamini Mungu kunirejesha, kimojawapo cha vitu vya kwanza nilichotambua ni kwamba ilibidi ule uhasi uondoke. Na ninapozidi kumhudumia Mungu, ninatambua nguvu kuu iliyo katika uchanya wa nia na maneno yangu.

Matendo yetu ni matokeo ya moja kwa moja ya mawazo yetu. Mawazo yaliyo hasi yatasababisha maisha hasi. Lakini tukigeuzwa na kufanywa upya nia zetu kulingana na Neno la Mungu, tuthibitishe katika maisha yetu “mapenzi yaliyo mema na yanayokubalika na yenye ukamilifu kwa Mungu” kama inavyoahidi Warumi 12:2.


Kulainisha mawazo yetu kuwiana na mawazo ya Mungu ni zoezi linalobadilisha maisha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon