Nguvu za Ajabu za Mungu Ndani Yako

Nguvu za Ajabu za Mungu Ndani Yako

Lakini ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu. Warumi 8:11

Kundi la wachungaji wakati mmoja liliniuliza swali lifuatalo: Kando na Mungu mwenyewe, ni kitu gani kimoja kilichokufanya kutoka mahali ulipoanzia katika huduma hadi kiwango cha mafanikio unachofurahia wakati huu? Punde tu nikasema, “Nilikataa kukata tamaa!” Kuna maelfu ya nyakati ambapo nilihisi kukata tamaa, nikafikiri kukata tamaa, na nikajaribiwa kukata tamaa, lakini wakati wote nilichuchumilia mbele tu. Ninamshukuru Mungu kwa azma anayotupatia.

Usiache maisha yakuponde—kabiliana nayo kwa ujasiri na ushupavu, na utangaze kwamba utafurahia kila kipengele chake. Unaweza kufanya hivyo kwa kuwa una nguvu za ajabu za Mungu zinazoishi ndani yako. Mungu huwa hafadhaiki wala kukata tamaa. Wakati wote huwa ana amani na furaha, na kwa kuwa anaishi ndani yetu, na tunaishi ndani yake, tunaweza kufurahia kitu hicho hicho. Tumwezeshwa na Mungu kwa ajili ya mambo magumu, na kwa usaidizi wake, hatuhitaji kukata tamaa!


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa kuwa kwa usaidizi wako, ninaweza kudhamiria kutokata tamaa. Ninaomba unipe ujasiri na ushupavu ninaohitaji ili kuchuchumilia mbele na kufanya ulichoniita kufanya. Asante kwa kuwa nguvu zako za ajabu zinaishi ndani yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon