Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. —1 YOHANA 4:11
Kupenda na kupendwa ndiko hufanya maisha yapendeze kuishi. Kupenda na kupendwa ndivyo vile Mungu alituumba—hupatia maisha kusudi na maana. Upendo ndio kitu kikubwa sana ulimwenguni.
Ni eneo linaloshambuliwa vikali pia katika maisha yetu. Lengo la shetani ni kututenga na upendo wa Mungu, na atatumia chochote anachoweza kutatiza ufahamu wetu wa upendo wa Mungu au autatanishe. Njia yake moja kuu ya udanganyifu ni kutufanya tuamini kwamba upendo wa Mungu juu yetu unategemea kustahili kwetu.
Hivi ndivyo ilivyotendeka katika maisha yangu: Wakati wowote nilipokosea, ningeacha kujiruhusu kupokea upendo wa Bwana na kuanza kujiadhibu kwa kuhisi kuhumika na kujilaumu. Niliishi hivi kwa muda mrefu wa maisha yangu, nikibeba mgongoni kama wajibu gunia langu la hukumu kila nilikoenda. Nilifanya makosa kila mara, na nikahisi kuhukumika kwa kila moja. Kisha ningejaribu kupata kibali cha Mungu kwa matendo mazuri.
Kwa shukrani, mwishowe siku ya uhuru ilifika kwangu. Mungu alinifunulia kwa neema kupitia kwa Roho Mtakatifu, upendo wake kwangu mimi binafsi. Huo ufunuo mmoja ulibadilisha maisha yangu yote na kutembea kwangu naye. Lilo hilo linaweza kukufanyikia. Unapogundua kwamba Mungu anakupenda bila masharti, kila kitu hubadilika. Unapendwa sio kwa sababu ya yale umetenda au hujatenda, lakini kwa sababu ya jinsi Mungu alivyo.
Upendo wa Mungu ni mtimilifu na usio na masharti. Unapokosea, anaendelea kukupenda kwa sababu upendo wake haukutegemei wewe ila Yeye.