Kuanza kwa Maombi

Ombeni bila kukoma [kuomba kwa uvumilivu]. —1 WATHESALONIKE 5:17

Nimekuwa nikitembea na Mungu kwa muda mrefu wa maisha yangu, na bado ninajifunza umuhimu wa kutokufanya kitu kabla ya kuomba kukihusu kwanza. Biblia inasema tuombe bila kukoma. Hii hamaanishi kwamba tukae tu siku nzima bila kufanya lolote isipokuwa kuomba. Inamaanisha tu kwamba, tuhusishe maombi katika kila kitu tunachofanya. Ninapenda kusema, “Ombea njia zako za siku.”

Maombi bila shaka ndiyo sehemu muhimu sana ya maandalizi ya maisha. Imesemekana kwamba kila kushindwa hufanyika kwa sababu ya kushindwa kuomba! Ninapendekeza kwamba usifanye lolote kabla ya kuomba kuanza.

Biblia inasema kwamba katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako (Mithali 3:6). Ni jambo kutia moyo kujua kwamba tunaweza kumwita Mungu na akatuongoza kila siku na kutupa nguvu.

Unamkaribia Mungu unapomwendea kwa maombi mchana kutwa. Inakuruhusu kushiriki na Mungu na kufungua milango kwake kufanya kazi katika maisha yako, hali yako, na maisha ya uwapendao.


Mungu atakuwezesha kufanya vitu ambavyo vitakushangaza kila mara ukimfanya mshiriki wako katika maisha. Lakini yote yanaanza kwa maombi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon