Kugeuza Hali Yoyote kwa ajili ya Wema

Kugeuza Hali Yoyote kwa ajili ya Wema

Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo. MWANZO 50:20

Chochote ambacho huenda kilitufanyikia hapo nyuma hakifai kuamua mustakabali wetu. Haijalishi kile ambacho huenda watu walijaribu kutufanyia, Mungu anaweza kukichukua na kukigeuza kuwa chema. Warumi 8:28 (BIBLIA) inasema, “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao…”

Katika Mwanzo 37–50, kaka za Yusufu walikusudia mabaya kinyume naye. Wakapanga mpango wa kuharibu maisha yake kwa kumuuza utumwani Misri. Lakini mwishowe, Yusufu akawa wa pili mamlakani baada ya Farao na akatumiwa na Mungu kuokoa maisha ya wengi.

Chochote kile kinachofanyika katika maisha yako, kumbuka kwamba Mungu yuko upande wako. Atayajenga maisha yako, sifa yako, familia yako na kazi yako. Kuwa mwenye shukrani kwamba yuko nawe, tia tumaini lako ndani yake, na uwe tayari kushangaa kuhusu vile anavyoweza kugeuza kila hali kwa ajili ya utukufu wake!


Sala ya Shukrani

Ninashukuru, Baba, kwamba unaweza kugeuza hali yoyote na kila hali katika maisha yangu kwa wema. Nisaidie leo kukutazama Wewe badala ya kutazama ya hapo nyuma. Na asante kwamba unaweza kuchukua hata sehemu zinazotesa sana za maisha na kuunda kitu chema kutokana nazo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon