Mabadiliko ni Kitu Kizuri

Lakini sisi sote kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho. —2 WAKORINTHO 3:18

Ningependa kukua na kuona mabadiliko, na nina hakika pia wewe. Ninataka kuona mabadiliko katika tabia yangu. Ninataka kuona nikipiga hatua mara kwa mara. Kwa mfano, ninataka uthabiti zaidi; ninataka kutembea katika kipimo kikuu zaidi cha upendo na matunda mengine yote ya Roho. Ninataka kuwa mwenye huruma na mwema kwa wengine, hata kama sijihisi vizuri au siku yangu haijakuwa nzuri. Hata kama vitu vinaenda kinyume nami na mambo hayaendi vizuri vile ningependa, bado ninataka kuonyesha tabia ya Yesu.

Kupitia kwa nguvu za Roho mtakatifu ndani yetu, tunaweza kuwa na furaha tele, kuwa wazuri na wenye huruma, hata kama vitu havituendei sawasawa. Tunaweza kukaa kwa utulivu wakati vitu vyote karibu nasi vinaonekana kuchanganyikiwa, wakati vitu vyote vimeungana kwenda kinyume nasi ili kutufanya tupoteze subira yetu na kukasirika pamoja na kusikitika.

Ufunguo wangu mwishowe umekuwa kujifunza kuwa Mungu hunibadilisha kupitia kwa neema yake, sio kupitia kwa kung’ang’ana kwangu ili nijibadilishe. Niliteseka kwa miaka mingi nikipigana na nafsi yangu kabla ya kutambua nguvu za Mungu zingenibadilisha kutoka ndani—hatua kwa hatua.


Hivi ndivyo Mungu anatubadilisha: Anatufunulia kitu halafu anangoja hadi tuamue kumwamini nacho kabla hajabadilisha sehemu hiyo ya maisha yetu polepole ili ifanane na tabia yake.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon