Jinsi ya Kuwa na Mabadiliko ya Kweli

Nguvu za Kuwa Mwenye Shukrani Tele

Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. 2 WAKORINTHO 4:16

Mabadiliko hayaji kupitia kwa kung’ang’ana, jitihada za binadamu bila Mungu, mfadhaiko, kujichukia, kujikataa, hatia au kazi za mwili. Mabadiliko katika maisha yetu huja kama matokeo ya nia zetu kufanywa upya na Neno la Mungu na kwa kumwamini Mungu kufanya kazi ndani yetu kulingana na mapenzi ya Mungu. Mungu aliyeanzisha kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza (tazama Wafilipi 1:6).

Tunapokubaliana na Mungu na kweli kuamini kwamba kile anachosema ni kweli, pole pole kinaanza kudhihirika ndani yetu. Tunaanza kufikiria kwa njia tofauti, halafu tunaanza kuongea kwa njia tofauti, na mwishowe matendo yetu yanakuwa tofauti. Huu ni mchakato unaojengeka kutoka hatua hadi nyingine, na lazima tukumbuke kila mara kwamba haya yanapoendelea, tunaweza kushukuru na kuwa na nia inayosema kwamba, “Mungu ananibadilisha kidogo kidogo, na ninaweza kufurahia anapoendelea kufanya kazi.”


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa kunibadilisha na kunifanya kile unachotaka niwe. Asante kwa kukamilisha kazi nzuri uliyoanzisha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon