Kufanya Kitu Kikubwa na Maisha Yako

Kufanya Kitu Kikubwa na Maisha Yako

Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana, basi chagua uzima ili uwe hai, wewe na uzao wako. Kumbukumbu la torati 30:19

Mara nyingi huwa ninawaza ni kwa nini watu wengine hufanya mambo makubwa na maisha yao huku wengine wakifanya machache au kukosa kufanya chochote. Ninajua kwamba matokeo ya maisha yetu hayamtegemei tu Mungu bali kitu pia ndani yetu. Kila mmoja wetu anafaaa kuamua iwapo atafika au hatafika chini ndani kabisa katika moyo wake na kupata ujasiri wa kuchuchumilia mbele na kusahau hofu, makosa, mateso mikononi mwa wengine, dhuluma, na changamoto zote ambazo maisha huwasilisha. Haya si mambo ambayo mtu mwingine anaweza kutufanyia; lazima tuyafanye wenyewe.

Ninakuhimiza kuyawajibikia maisha yako na matokeo yake. Kuwa mwenye shukrani kwa baraka za Mungu za zamani na umwamini hata kwa zingine zaidi katika siku zijazo. Utafanya nini na kile Mungu amekupa? Mungu humpa kila mtu nafasi sawa—unaweza kuchagua uzima au mauti (tazama Kumbukumbu la Torati 30:19). Chaguo ni lako, na ninaamini kwamba utafanya uamuzi ufaao!


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwa nafasi ya kukufanyia mambo makubwa. Ninaomba kwamba utanisaidia kuitumia vizuri kila siku mpya. Asante kwa kuwa ninaweza kuota ndoto kubwa. Na kwa sababu uko nami hakuna kisichowezekana.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon