Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele. —WAEBRANIA 13:8
Ni kitu gani kikubwa ambacho tunapenda kuhusu Yesu? Kuna majibu mengi sana kwa swali hilo, bila shaka, kama ukweli kwamba alitufia msalabani ili tusipate adhabu kwa dhambi zetu; halafu akafufuka siku ya tatu. Lakini katika uhusiano wetu wa kila siku naye, mojawapo ya vitu ambavyo tunatambua sana kumhusu ni ukweli kwamba tunaweza kutegemea kutobadilika kwake. Anaweza kubadilika kitu kingine chochote anachohitaji kubadilisha, lakini yeye mwenyewe hubaki vilevile.
Hiyo ndiyo aina ya mtu ambaye tunaweza kutazamia kuwa, lakini haitawahi kufanyika iwapo hatutaweza kudhibiti hisia zetu. Kukomaa kihisia kuna maana ya kufanya uamuzi kwa kutegemea uongozi wa Roho Mtakatifu, sio kwa hisia zetu. Lakini haifanyiki kikawaida.
Hisia zetu hazitawahi kuondoka, lakini tunaweza kujifunza kuzidhibiti. Mungu ana uwezo wa kutuleta katika kiasi. Haimaanishi tukose hisia au tusiwe wachangamfu. Mungu alitupatia hisia ili tufurahie maisha. Lakini inamaanisha tujidhibiti katika nguvu na uwezo wa Roho Mtakatifu tunapoongozwa naye.
Mungu hataki tubadilike kila mara hali zetu zinapobadilika. Anataka tubaki vilevile, jinsi alivyo.