Mungu Hukufahamu

Hakuna afahamuye; hakuna mtu amtafutaye Mungu. —WARUMI 3:11

Mtu yeyote anayeamua kumfuata Mungu kwa karibu atakuwa na nyakati za kutoeleweka na watu ambao hawajitolea vivyo hivyo. Watu wasio na imani hawawaelewi watu walio na imani!

Wakati wote kutakuwa na wale ambao hawatajua watakachofikiria kutuhusu tunapojisalimisha kwa Mungu. Vilevile watu hawakujua la kufikiria kuhusu Yesu. Kwa kweli hakuna aliyemwelewa au kuelewa mwito uliokuwa juu ya maisha yake, sio hata familia yake.

Tunapokosa kusema au kufanya vile watu wengine wanasema na kufanya kwa sababu tumeamua kumfuata Mungu badala ya ulimwengu, huenda tukakosa kueleweka na hivyo kukataliwa. Inaumiza hilo likifanyika, laikini wakati wote kukumbuka kwamba Yesu hakukatai, na hilo ndilo muhimu kweli.

Huenda utiifu wako wa Mungu ukamaanisha kwamba hutatoshea katika udhibiti wa mambo ya mara kwa mara yanayoendelea katika mazingira yao. Huenda ukahisi umetengeka wakati mwingine, lakini katika nyakati hizo kumbuka kwamba Mungu atatuza uaminifu wako. Anakupenda, na wakati ule watu wengine wanauliza “Nini kibaya nawe?” Mungu atakuwa anasema, “Hakuna kitu kibaya nawe. Wewe ni wangu na ninakuonea fahari.”


Fanya uamuzi kusimama na Mungu na kufanya anachosema, hata kama hakuna anayeelewa wala kuunga mkono. Yesu anakuelewa na anatosha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon