Mungu Huzungumza Faraja na Utulizo

Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote (2 WAKORINTHO 1:3)

Sisi wote hutamani kukubalika sio kukatawaliwa. Ninachukia hisia za upweke na uchungu ambazo hutokana na kuhisi kukataliwa, ilhali niliipitia hayo kwa muda wa miaka mingi, bila kujua ningefanya jambo kuhusu hilo. Ninashukuru Mungu kwamba hayo yote yamebadilika!

Miaka mingi iliyopita, kitu kilifanyika ambacho kiliregesha uchungu wa kale wa kukatawaliwa. Nilimsamehe mtu ambaye alikuwa amenidhuru sana utotoni. Badala ya msamaha, nililaumiwa kwa kitu ambacho hakikuwa kosa langu na nikapokea ujumbe dhahiri kwamba mtu huyu hakuwa na haja yoyote nami kabisa.

Nilikuwa ninataka kujificha na kujihurumia, lakini badala yake, nilimwomba Mungu faraja za Roho Mtakatifu mara moja. Nilimwomba kuponya hisia zangu zilizojeruhiwa na kuniwezesha kushughulikia hali hii jinsi Yesu angeishughulikia. Nilipoendelea kumtegemea Mungu, Nilihisi joto likinifinika, karibu kama vile mafuta ya kutuliza yanavyomwagwa juu ya vidonda vyangu.

Nilimwomba Mungu amsamehe mtu ambaye alikuwa amenidhuru, na akaleta mawazoni mwangu msemo kwamba, “Watu wanaodhurika hudhuru wengine.” Majibu yake ya ndani na ya kibinafsi yalileta uponyaji katika roho yangu iliyokuwa imejeruhiwa.

Mungu ndiye chanzo cha faraja zote, utulizo na himizo. Tafadhali fanya lolote uwezalo kuanzisha na kudumisha uhusiano wa ndani na Mungu kwa sababu huo ndio muktadha ambamo utaweza kusikia sauti yake, kupokea faraja zake na uponyaji, na kutiwa nguvu na himizo na utunzi wake.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Mungu anajua jinsi ilivyo muhimu kufarijiwa; Alikutumia Roho Mtakatifu kufanya tu hilo.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon