Basi tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? [Ni nani anayeweza kuwa adui yetu, akiwapo Mungu upande wetu?) —WARUMI 8:31
Mungu ni Mungu mkuu; hakuna asiloliweza. Hatuna la kuogopa kutoka kwa adui zetu kwa sababu hakuna mmoja wao aliye mkuu kuliko Mungu wetu.
Mungu yuko nasi, yuko upande wetu. Shetani ana nafasi moja- yuko kinyume chetu. Lakini Mungu yuko juu yetu, chini yetu, kupitia kwetu, upande wetu, na anatuzunguka. Basi tutamwogopa nani?
Kwa hivyo kama Mlima Zayuni, hatufai kutingizika kwa sababu Mungu yuko Mungu anatuzunguka kila mahali. Na kama ambayo haikutosha, nilitaka niseme jambo zuri kabisa mwishoni: Yuko ndani yetu, na alisema kwamba hatatuacha wala kutusahau. Wokovu ni baraka ya heshima sana kwetu kutoka kwa Mungu, na tumepewa Msaidizi, Roho Mtakatifu mwenyewe, kutuwezesha kuwa kama Yesu. Mungu ana baraka na nguvu za kiroho kwa wingi kwetu sisi. Ni mwenye uwezo na nguvu na anayeweza kufanya tusiyoweza kufanya peke yetu.
Mungu hutamani turuhusu Roho Mtakatifu atiririke kupitia kwetu katika nguvu ili kuonyesha watu upendo wake na kusaidia watu kwa vipawa vyake. Yote haya yako ndani yake.
Mungu huchagua vitu dhaifu na vipumbavu vya ulimwengu huu, kimaksudi, ili watu waviangalie na kusema, “Lazima awe ni Mungu!”