Neno la Mungu Huathiri Kila Eneo la Maisha Yetu

Neno la Mungu Huathiri Kila Eneo la Maisha Yetu

Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu. ZABURI 119:105

Mawazo, maneno na hisia hasi, na mahusiano yanaweza kusababisha mfadhaiko—na mfadhaiko unaweza kusababisha ugonjwa—fikra chanya, maneno, hisia, na mahusiano yanaweza kuleta afya na uponyaji. Fikiria kuhusu Maandiko yafuatayo:

“Moyo uliyo mzima ni uhai wa mwili; bali husuda ni ubovu wa mifupa…” (Mithali 14:30)

  • “Mwanangu, sikiliza maneno yangu…maana ni uhai kwa wale wazipatao, na afya ya mwili wao wote.” (Mithali 4:20,22)
  • “Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; ni tamu nafsini, na afya mifupani (Mithali 16:24)
  • Tunaweza kushukuru kwa nguvu za Neno la Mungu katika maisha yetu. Kutafakari Andiko na kufuata maagizo ya Mungu hutusababisha kufikiria, kuongea, na kuishi kwa njia ambayo huleta uponyaji kwa kila sehemu ya maisha yetu.

Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwa Neno lako na uponyaji linaloleta kwa maisha yangu. Ninashukuru kuwa fikra, maneno, hisia na mahusiano yangu hubadilishwa na uongozi unaonipa kupitia kwa Andiko.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon