Unapohisi kuwa na Wasiwasi

Unapohisi kuwa na Wasiwasi

Kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito…ili atukuzwe… — ISAYA 61:3

Mungu anataka kutushughulikia, lakini ili tumruhusu, ni muhimu kwamba, tuchague kuacha kuwa na wasiwasi. Watu wengi wanasema wanataka Mungu awashughulikie, lakini wanaishi siku zao zote kwa wasiwasi au kujaribu kutafuta suluhu za matatizo yao badala ya kungoja mwelekeo kutoka kwa Mungu. Kwa kweli wanagaragara katika “majivu” yao, lakini bado wanataka Mungu awape urembo. Ili Mungu atupe urembo, lazima tumpe “majivu.”

Tunampa Mungu fadhaa zetu kwa kuamini kuwa anaweza na atatushughulikia. Waebrania 4:3 inasema, “Maana sisi tulioamini (kushikilia, kuamini na kutegemea Mungu) tunaingia katika raha ile…”

Tunaingia katika raha ya Mungu kupitia kwa kuamini. Wasiwasi ni kinyume cha imani. Wasiwasi huiba amani yetu, kutudhoofisha kimwili, na inaweza hata kutufanya tuwe wagonjwa. Iwapo tuna wasiwasi, ina maana kwamba hatumwamini Mungu na kwa hivyo hatutaingia katika raha yake.

Biashara ilioje ambayo Mungu ameleta. Unampa majivu, na anakupa urembo. Unampa wasiwasi wako wote na yanayokujalisha, na anakupa ulinzi, uthabiti, mahali pa kujificha, na furaha kamilifu—faida ya kushughulikiwa naye.


Yesu hakuwa na wasiwasi, na huna lazima ya kuwa na wasiwasi pia.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon