Na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na mwana wake Yesu Kristo (1 YOHANA 1:3)
Mungu anataka ushirika nasi. Katika andiko la leo, Yohana anaandika kuhusu ushirika wake na Baba pamoja na Mwana, na katika 2 Wakorintho 13:14, Paulo anaandika kuhusu ushirika au umoja na Roho Mtakatifu. Umoja wa Roho Mtakatifu unarejelea ushirika wetu na waaminiyo wengine na Roho mwenyewe. Kwa kuwa Roho Mtakatifu anaishi ndani yetu, si lazima twende mbali ili tuwe na ushirika na umoja naye.
Pengine mfano mzuri wa nitakaotumia kueleza ushirika ni ule wa watu wawili wanaoishi pamoja, kama vile mke na mume. Ninaishi katika nyumba na mume wangu, Dave, na tuko karibu sana. Tunafanya kazi pamoja na kufanya vitu vingine vingi pamoja. Kuna wakati amabo yeye huenda kucheza gofu, lakini tunakaa karibu kupitia kwa simu. Huenda akatazama michezo kwenye runinga, na hata ingawa huwa hainifurahishi, bado niko ndani ya nyumba. Dave na mimi hula chakula pamoja, kulala pamoja na kutumia bafu pamoja asubuhi tunapojiandaa kwenda kwenye shughuli za siku. Tunatumia wakati mwingi tukiwa pamoja. Hatuzungumzi kila mara, lakini huwa tunajuana kila wakati. Tunapokuwa na hizo nyakati tulivu huwa tunawasiliana sana. Ninamwambia Dave kuhusu vitu vilivyo muhimu kwangu na vitu visivyo muhimu. Anafanya hivyo hivyo pia. Mmoja wetu anapozungumza, yule mwingine husikiliza.
Kwa njia rahisi, ushirika unahusu kuwa pamoja, mkizungumza na kusikiliza. Roho Mtakatifu huwa nasi kila wakati. Anaishi ndani yetu na hayuko kando nasi. Tunaweza kuzungumza naye na atasikiliza. Na atazungumza nasi, kwa hivyo tunahitaji kusikiliza.
NENO LA MUNGU KWAKO LEO:
Jifunze kutulia na Mungu. Mchukue kama mgeni mashuhuri katika nyumba yako.