Yesu Pekee

Katika ungwana huo, Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa (ambalo mmeliondoa) —Wagalatia 5:1

Yesu alikuja katika ulimwengu huu na akalipia dhambi zetu, akajitwika adhabu yetu mwenyewe. Akawa kibadala chetu, akalipa deni tulilodaiwa, bila sisi kugharimika. Alifanya haya yote bila malipo kwa sababu ya upendo wake mkuu, neema na huruma.

Yesu alirithi vyote ambavyo Baba alimrithisha na akatuambia kuwa sisi ni warithi pamoja naye kutokana na imani yetu. Ametwaa njia ya ushindi wetu mkamilifu hapa na hata baadaye. Ameshinda na tunapata thawabu bila kuilipia. Sisi tu zaidi ya washindi.

Itarahisishwa vipi zaidi? Injili ni rahisi ajabu.

Kutatanisha mambo ni kazi ya Shetani. Anachukia urahisi kwa sababu anajua nguvu na furaha ambayo imani yetu huleta. Uhusiano wako na Mungu unapokuwa na utata, rudia wepesi wa kuamini kama mtoto mdogo. Yesu alisema, “amini tu” na utaona utukufu wa Mungu (Yohana 11:40).

Rudi usherehekee wepesi wa imani yako katika Yesu pekee.


Kuamini ni rahisi sana kuliko kukosa kuamini.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon