Kristo Ndani yako, Tumaini la Utukufu

Ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu. —WAKOLOSAI 1:27

Wewe na mimi tunaweza kutambua na kuwa na utukufu wa Mungu katika maisha yetu kwa sababu ya Yesu ndani yetu. Ni tumaini letu la kuona vitu bora zaidi.

Utukufu wa Mungu ni ufanisi wake unaodhihirika. Kama wana wa Mungu, tuna urithi ndani ya Yesu, kibali cha kuishi katika ufanisi wake unaodhihirika. Shetani hupigana kwa hasira ili atudanganye. Anataka tuamini hatuwezi, hatustahili, na tumekataliwa katika kupata mema ya Mungu. Ndiyo kwa sababu wengi hujitazama na kuhisi kushindwa.

Lakini iwapo utakumbuka kwamba kwa sababu ya Kristo ndani yako, unaweza kushuhudia utukufu wa Mungu—wema wa Mungu unaodhihirika—utaishi ukiwa mwingi wa tumaini. Utachuchumilia mbele kwenye vitu bora zaidi kila siku ya maisha yako. Usitazame tu yale unayoweza kufanya bali lenga kutazama yale Mungu anaweza kufanya kupitia kwako.

Je, uko tayari kumwamini Mungu kukumwagia wema na ufanisi wake katika maisha yako!


Mema ya Mungu yako njiani, kwa hivyo furahia na utarajie vitu vizuri!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon