Mungu Husikia na Huelewa

Mungu Husikia na Huelewa

Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. —1 YOHANA 5:14

Maombi ni mojawapo ya vitu vinavyoakisi ukaribu wetu na Mungu na hakika yetu ndani yake. Tukiomba kuhusu kila kitu badala ya kuwa na wasiwasi na kujaribu kujifanyia, tunasema kwa nia na matendo yetu, “Bwana, ninakutumainia katika hali hii.”

Ninaamini wengi wetu tunaomba kisha tunashangaa iwapo Mungu amesikia. Tunashangaa iwapo tuliomba vizuri kwa muda mrefu wa kutosha. Tunashangaa iwapo tulitumia vifungu vizuri vya maneno, maandiko ya kutosha, na kadhalika. Hatuwezi kuomba vizuri tukiwa na shaka na kukosa kuamini. Maombi huhitaji imani.

Mungu amekuwa akinihimiza kutambua kwamba maombi rahisi yaliyojaa imani hufanya kazi. Sina lazima ya kurudiarudia vitu. Sina haja kuwa kupamba lugha yangu. Ninaweza tu kuwa mimi na kujua kwamba ananisikiliza na kunielewa.

Ninakuhimiza kuwasilisha tu maombi yako na kuamini kwamba Mungu amekusikia na atajibu kwa wakati mzuri. Kuwa na hakika unapoomba. Jua kwamba Mungu husikia na anafurahishwa na maombi rahisi kama ya mtoto yanayotoka katika moyo mwaminifu.


Mtumainie Mungu kujibu maswali yako kwa njia yake na katika wakati wake mtimilifu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon