Jifunze Kujipenda

Jifunze Kujipenda

. . . Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu. —YEREMIA 31:3

Kwa kweli watu wengi hawajipendi, Ni wenye kujikosoa: hujikataa na huenda hata wakajichukia. Biblia inatufundisha tusiwe na choyo na wenye nafsi ya kujifikiria, lakini haikuwahi kutuagiza kutokujipenda kwa kiasi. Kila mara huwa ninasema, “Usiwe katika mapenzi na nafsi yako lakini jipende.” Usipojipenda, utaishi kwa dhiki kwa sababu mara nyingi uko na wewe. Wewe ni mtu mmoja ambaye huwezi kuacha, sio hata kwa sekunde moja ya maisha yako.

Wakati mmoja nilisikia mwanamke mdogo akimwuliza mchungaji kumwombea kwa sababu alijichukia. Alimwangalia na kuchukua hatua moja nyuma kwa mshangao. Akasema dhahiri, “Unafikiria wewe ni nani kujichukia baada ya Mungu kumtuma Mwanawe wa pekee kuteseka vibaya hivyo na kufa mahali pako? Kama Mungu alikupenda sana hivyo, kwa hakika unaweza kujipenda.”

Taarifa yake ilimfungua macho kwa kosa alilokuwa akifanya, na akaanza safari yake ya kujifunza kujipenda na kujikubali. Ninakuhimiza kufanya vilevile. Chukua hatua ya imani na useme, “Ninajipenda kwa upendo wa Mungu. Ninajikubali.”

Unapoanza kujiona vile Mungu anavyokuona, mwelekeo wako wote na tabia mtazamo utabadilika. Utakuwa mtu mwenye fikra chanya zaidi na mkakamavu, na utaanza kufurahia maisha yako zaidi.


Kwa sababu Mungu anakupenda, unaweza kujipenda.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon