Aina Tofauti za Kibali

Aina Tofauti za Kibali

Na uzuri wa Bwana, Mungu wetu, uwe juu yetu. Na kazi ya mikono yetu utufanyie thabiti, naam, kazi ya mikono yetu uithibitishe. —ZABURI 90:17

Kuna tofauti kati ya kibali cha kawaida na kibali cha kimiujiza. Kibali cha kawaida kinaweza kuchumwa, ilhali kibali cha kimiujiza hakiwezi.

Ukifanya kazi kwa bidii na kwa masaa marefu ya kutosha, unaweza kupata watu wa kukupenda na kukukubali wakati mwingi. Lakini lazima kukukubalika huko kuendelezwe vile kulikopatikana. Kulazimika kusema na kufanya vitu vyote vinavyofaa kila wakati ili kukubalika na watu ni aina ya utumwa.

Iwapo tutachagua kumfuata Mungu badala ya watu, atatupatia kibali chake. Ni kipawa cha neema yake na haiwezi kuchumwa. Mungu hataki tuharibu muda na nguvu zetu kwa kujaribu kuchuma kibali; anataka tumtumainie kukipata. Mungu anapotupatia kibali chake, vitu vya ajabu vinaanza kufanyika. Milango ya nafasi inaanza kukufungukia. Utaishia kuwa na faida na baraka ambazo hujachuma wala kustahili kupewa

Tunaweza kuomba kila siku kuhusu kibali cha Mungu cha kimiujiza. Ni kipawa cha Mungu ambacho huja kwa neema kupitia kwa imani yetu. Endelea kuomba, na uendelee kuomba na utapokea!


Tunapojua kwamba kila kitu tulicho nacho na tunachofurahia ni kipawa kutoka kwa Mungu, matokeo ya kibali chake cha kimiujiza juu yetu, basi hakuna lingine la kufanya isipokuwa kusema, “Asante Bwana.”

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon