Chagua Uzima Wakati Wote

Chagua Uzima Wakati Wote

Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. — WARUMI 8:6

Hali nzuri kabisa kwa nia zetu vile Paulo alieleza katika Wafilipi 4:8—yaliyo safi, ya kupendeza na kupendeka, ya huruma, ya haki na neema, yatafakarini mambo yenye sifa njema na wema. Hii ndiyo maana ya kuwa na nia ya Kristo. Ninapenda kuwakumbusha watu kwamba ni muhimu tufikirie kuhusu tunachofikiria.

Watu wengi kwa kupotoka hufikiri kwamba chanzo cha dhiki au mashaka yao ni kitu kingine cha kando. Wanalaumu hali ya nje ilhali ni mawazo yao ya ndani ambayo yanawasababishia dhiki. Lakini iwapo tutachagua “kuchungana” na mawazo yetu, tunaweza kuiteka nyara kila fikra ipate kumtii Yesu Kristo (2 Wakorintho 10:5).

Sehemu kubwa ya kumkaribia Mungu ni kusalimisha fikra zetu kwake. Tutakapofanya hivi, Roho Mtakatifu ni mwepesi kutukumbusha iwapo fikra zetu zimeanza kutuelekeza upande mbaya. Uamuzi basi huwa wetu—iwapo tutaendelea kuelekea upande huo au tutachagua kufikiri na nia ya Yesu? Njia moja ya kufikiria huelekea katika masikitiko, ubaya na kupoteza tumaini, nyingine huelekea kwenye uzima. Chagua uzima leo!


Fikra zako, maneno yako, nia zako, na matendo yako yote ni matokeo ya uteuzi unaofanya kila siku.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon