Furaha na Kila Hatua Mpya

Furaha na Kila Hatua Mpya

. . .Kama kuumaliza mwendo wangu kwa furaha. MATENDO YA MITUME20:24

Mtume Paulo alitaka kuwa kile chote Mungu alitaka awe, na akatamani kufanya yote ambayo Mungu alitaka afanye—lakini alitaka kuyafanya kwa furaha. Tunafaa kujifunza kuwa na furaha kuhusu maendeleo yetu, sio kufadhaika kuhusu ule umbali ambao bado tunahitajiwa kwenda au kukandamizwa na mtazamo wa kisheria kuhusu hilo. Tunaweza kushukuru kwa kila kitu ambacho Mungu amefanya na kila ambacho bado atafanya. Tunaweza kujifunza kutazama yaliyo chanya na sio yaliyo hasi.

Mojawapo ya athari za kumtazama Mungu kisheria ni kwamba watu hawawezi kuridhika hadi watii sheria zote. Wakikosea kwa moja, wanakosa juu ya yote (tazama Yakobo 2:10). Maisha wakati mwingine hujawa na kushindwa, masikitiko na mfadhaiko. Lakini mojawapo ya faida za uhusiano wa Agano Jipya na Yesu ni ukweli kwamba tunaweza kuongozwa na Roho Mtakatifu badala ya kanuni, na tunaweza kufurahi wakati wa safari. Furaha yetu haistahili kupatikana katika matendo yetu, lakini ndani ya Yesu mwenyewe.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba unanipa furaha ya safari. Hata ninapojifunza na kukua ndani yako, ninaweza kuwa na furaha kila siku mpya. Asante kwamba sihitaji kuishi chini ya sheria; ninaishi katika neema yako na furaha yako katika kila hatua njiani.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon