Hakuna Kulalamika Tena

Hakuna Kulalamika Tena

Mhimidini Bwana, enyi majeshi yake yote, ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake. ZABURI 103:21

Tukidumisha mtazamo wa kutoa shukrani, tutafunga mlango wa manung’uniko na malalamiko—ambayo huwa ni majaribu yaliyo katika maisha yetu kila wakati. Ukweli ni kwamba huwa hatuanzi tu kuwa na tabia ya kulalamika; sisi wote tulizaliwa nayo. Lakini kwa usaidizi wa Mungu, tunaweza kuanza kuwa na tabia ya kushukuru na kuikuza.

Tukizoea kila mara kusifu, kuabudu, na kumshukuru Mungu, hakutakuwa na nafasi ya kulalamika, kutafuta makosa, na kunung’unika. Biblia inasema katika Wafilipi 2:14: “Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano…” Kulalamika hufungua mlango kwa shetani kusababisha mashaka, lakini shukrani hufungua mlango kwa Mungu ili atubariki.


Sala ya Shukrani

Ninashukuru, Baba, kwamba kwa usaidizi wako, ninaweza kukuza fikra za shukrani. Ninakuabudu kwa sababu ya wema wako, uwezo wako na nguvu zako. Ninachagua kuwa mwenye shukrani kwa ajili ya uwepo wako katika maisha yangu badala ya kunung’unika na kulalalmika kuhusu mambo duniani.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon