hekima inakuita

hekima inakuita

Juu ya mahali palipoinuka karibu na njia, Penye njia panda, ndipo asimamapo. Karibu na malango, mahali pa kuingia mjini, Mahali pa kuyaingilia malango anapiga kelele. Mithali 8:2-3

 Katika safari yetu maishani, tutatakiwa kufanya maamuzi mengi, na daima tutaingia kwa shida ikiwa tunafanya kihisia au kulingana na kile tunachofikiri au tunachotaka.

Mungu anataka tufanye maamuzi ya busara. Ninaamini kwamba kuwa na hekima ni kuchagua kufanya sasa kile kitakacholeta furaha baadaye.

Mithali inasema kuwa hekima inatuita sisi. Lazima uende katika hekima ya Mungu na ujue kwamba uchaguzi uliofanya leo utaathiri kesho yako. Watu wengi hawafurahii maisha kwa sababu daima wanakabiliana na fujo kutokana na ukosefu wa hekima.

Usifanye kitu cha ubinafsi, ukidhani kwamba mambo yatatokea vyema. Hekima haina utani; inawekeza kwa siku za usoni. Hekima haipatikani kwa furaha ya papo hapo. Badala yake, inamfuata Mungu kwa siku njema za mbeleni.

Je wewe? Je! Unatembea katika hekima leo? Ikiwa sivyo, habari njema ni kwamba hekima tayari inakuita. Mungu yuko tayari na anangoja kukupa hekima yake. Muulize tu na ufanye maamuzi ambayo yatawekeza katika maisha ya baadaye.

 OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, nataka kufurahia maisha, sio kushughulikia mara kwa mara matatizo ambayo yanatokana na ukosefu wa hekima. Asante kwa kutoa hekima yako kwangu. Mimi nachagua kupokea na kufanya maamuzi ya kimungu juu ya maisha yangu ya baadaye.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon