Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya pamoja na tamaa zake. WAGALATIA 5:24
Hisia ni kigeugeu sana. Hubadilika wakati wote; huja na kwenda kama mawimbi ya baharini. Yanaenda juu, kisha chini, na kuonekana kudhibitiwa na nguvu zisizoonekana ambazo hatuelewi. Tukiwa na hekima hatutaenda safari katika bahari iliyovurugika kwa mawimbi yanayoonekana kuwa hatari, na hatufai pia kufuata hisia zetu zinapobadilika kwa kuvurugika.
Shukuru kuwa si lazima tudhibitiwe na hisia zetu. Tunaweza kujisalimisha kwa Neno la Mungu badala yake. Kitu kizuri unachoweza kufanya unapokuwa na hisia kupita kiasi, ni kusubiri hisia zako zitulie kabla hujachukua hatua yoyote. Chukua kasia na uendeshe dau lako. Usiingie dauni bila mtu wa kushika kasia na utumai tu kwamba mawimbi ya maisha yatakupeleka mahali fulani pazuri. Badala ya kufuata hisia, mwamini Mungu na ufuate Neno lake iwapo kweli unataka kuwa na maisha yaliyojaa furaha.
Sala ya Shukrani
Baba, ninakushukuru kwa kipaji cha Neno lako. Ninashukuru kwamba sihitaji kuishi nikiwa nimedhibitiwa na hisia zangu. Ninachagua badala yake kuishi kulingana na ahadi na maagizo yaliyo katika Neno la Mungu.