Imani Na Neema

Imani na Neema

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. —Waefeso 2:8–9

Ni ajabu kugundua kuwa wokovu huja kwa neema bure ya Mungu na inaweza kupokewa kwa urahisi kupitia kwa wepesi wa imani ya kitoto. Kwa shukrani, hatutakiwi kuufanyia kazi wokovu wetu kwa sababu tayari Yesu alikwishafanya kazi yote. Tunaupokea kwa imani peke yake! Ninaamini kwamba vile tunavyopokea msamaha wa dhambi na maisha ya milele, ndivyo tunavyofaa kuishi maisha yetu ya kila siku. Tunafaa kuchanganya imani yetu na kila kitu tunachofanya.

Imani ni kuegemea kwa nafsi yote ya mwanadamu kwa Mungu katika imani na tumaini kamilifu katika nguvu, hekima na wema wake. Tunapopitia maisha tukimwegemea katika kila kitu, atatuongoza wakati wote na kutupatia nguvu na uwezo wa kufanya tunayohitaji kufanya. Habari njema ni kwamba haulazimiki kujaribu kufanya mambo mwenyewe!

Mungu amemtuma Roho Mtakatifu ambaye ni msaidizi wako, kwa hivyo itisha na upokee usaidizi unaouhitaji leo na kila siku, na utulie katika upendo, huruma na neema.


Badilisha hofu, wasiwasi na fadhaa zako na imani rahisi na ufurahie siku yako!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon