Je, Imani Yako Inafanya Kazi?

Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo (WAGALATIA 5:6)

Watu wengi hufikiri imani kuu ndiyo ishara ya kwanza ya ukomavu wa kiroho, lakini ninaamini kipimo cha kweli kabisa cha ukomavu wa kiroho ni kutembea katika upendo. Kutembea kwetu kwa upendo huipa imani yetu nguvu. Hatuwezi kuwa na uhusiano mzuri na Mungu bila kuwa imani ndani ya Mungu, lakini upendo hudhihirisha, huwezesha, na kueleza imani yetu. Iwapo kweli tunampenda Mungu na kuwa na imani ndani yake, tutawapenda watu pia.

Andiko la leo linatufundisha kuwa imani hufanya kazi kupitia kwa upendo, na upendo sio tu mazungumzo wala nadharia; ni matendo. Kwa kweli Biblia inasema kwamba hatuwezi kuwa tunatembea katika upendo tukiona ndugu mhitaji na tuna vile tunavyoweza kutimiza haja yake na tukose kumsaidia (soma 1 Yohana 3:17).

Yesu pia akasema sheria yote na manabii wote wanazungumza kuhusu huu upendo alipotangaza: “Mpende Bwana wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.” Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii (Mathayo 22:37-40)

Yesu aliwapa maneno haya watu waliokuwa wakitaka kujua amri iliyokuwa kuu. Kimsingi walimwambia: “Tupatie tu msingi Yesu.” Akajibu: “Sawa, mnataka msingi? Mnataka kutii sheria yote kikamilifu na manabii wote? Basi nipendeni na mpende watu.” Ni rahisi hivyo. Yesu aliwajulisha watu kwamba kutembea katika upendo ndio ufunguo wa kuishi maisha yanayompendeza. Kujaribu kutembea katika imani bila upendo ni kama kuwa na tochi isiyokuwa na betri. Lazima tuhakikishe kwamba betri ya upendo wetu ina nishati kila mara. La sivyo imani yetu haitafanya kazi!

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Mungu ni upendo na tunavyozidi kumjua ndivyo tutawapenda wengine.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon