Kaa Mahali Pako

Kaa Mahali Pako

Yehoshafati akainama kichwa, kifudifudi wakaanguka mbele za Bwana, Yuda wote na wakaao Yerusalemu, wakimsujudia Bwana. —2 Mambo Ya Nyakati 20:18

Katika Mambo ya Nyakati 20:18, mfalme na watu wa Yuda waliinama vichwa, nyuso zao kifudifudi kwenye ardhi chini na kuabudu waliposikia maagizo ya Bwana. Mahali pa kuabudu Mungu palikuwa panawasaidia kujitayarisha kwa vita. Iwapo uko vitani sasa hivi, ninakuhimiza kwa msisitizo kubadilisha wasiwasi wote na ibada. Kupiga magoti kwa heshima mbele za Mungu, au aina nyingine za ibada, ni pahali pa vita na ufunguo wa nguvu za kiroho.

“Kusifu” Mungu kumefafanuliwa kama kumtunukia utukufu unaostahili jina lake. Ni kuzungumza na kuimba kuhusu wema, neema, na ukuu wa Mungu. “Kuabudu” kumefafanuliwa kama kutwaa heshima na kutumikia. Kwa mapana, inaweza kuchukuliwa kama utambuaji wa moja kwa moja wa Mungu, wa jinsi alivyo, sifa zake, njia zake na madai, kwa kujieleza kwa moyo wako kupitia kwa sifa na kutoa shukrani au, kwa matendo yanayofanywa kwa kutambua hayo.

Kwa usaidizi wa Mungu, tunaweza kujifunza kupigana vile anavyopigana sio kwa njia ya ulimwengu. Mahali petu pa vita ni pa ibada, na hapa ni pahali panapotuleta karibu na Mungu. Tunapigana kila vita kwa moyo wa sifa na ibada, tukiamini kwamba Mungu atafanya kazi katika maisha na hali zetu.


Tunapomwabudu Mungu, tunaachilia mzigo wa kihisia au kiakili unaotufunga nira. Unamezwa katika wema wa Mungu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon