Kile Mungu Anasema Kukuhusu

Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo mpendwa. —WAEFESO 1:6

Sio matamanio ya Mungu kwetu sisi kuhisi kutamauka na kuhukumika katika maisha yetu. Anataka tutambue kwamba sisi ni wanawe, na tunapendeza kwake.

Kuna sauti nyingi zinazojaribu kutuambia tulicho na tusicho, lakini kadri tunavyomkaribia Mungu, ndivyo tunavyosikia zaidi akituambia sisi ni akina nani—wenye haki ndani ya Yesu, tunaopendwa na kumpendeza Baba yetu wa mbinguni.

Shetani anatuambia huenda hatukubaliki na Mungu kwa sababu ya dhambi na makosa yetu, lakini Mungu anatuambia, kwamba tumekubalika ndani ya mpendwa kwa sababu ya kile Mwanawe, Yesu, amefanya tayari.

Iwapo umekabiliana au unakabiliana na lawama au hukumu leo, kumbuka kwamba Mungu huwa hatukumbushi jinsi tulivyoanguka. Kila wakati huwa anatukumbusha vile tunavyoweza kuinuka. Hutukumbusha jinsi tulivyoshinda, jinsi tulivyo wenye thamani machoni pake, na vile anavyotupenda.


Kadri unavyotembea na Mungu, ndivyo unavyohisi vizuri zaidi kuhusu mtu aliyekuumba kuwa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon