Kimbia Mbio Zako

Kimbia Mbio Zako

Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa subira katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu. —Waebrania 12:1

Iwapo tutakimbia mbio zetu katika maisha, iwapo tutatimiza kusudi letu na kutenda mapenzi ya Mungu, ni muhimu kuweka kando kila nira na dhambi na kukimbia mbio hizo kwa uvumilivu. Katika siku ambazo msitari huu uliandikwa, wakimbiaji walishurutisha miili yao kukimbia vile tu tufanyavyo leo. Lakini wakati wa kukimbia walivua nguo zote isipokuwa nguo ya kiuno, ili wakikimbia pasiwe na chochote cha kuwazuia. Waliipaka miili yao mafuta laini pia.

Katika maisha yetu ya Ukristo, tumeitwa kuondoa kitu chochote kinachotuzuia kukimbia mbio ambazo Mungu ameweka mbele zetu. Ni muhimu kuwa tumepakwa, au kuwa na upako, wa Roho Mtakatifu (mara nyingi huwakilishwa na mafuta) wa iwapo tutaenda kushinda mbio zetu.

Shetani ana njia nyingi za kututega na kutuzuia kuishi katika utiifu kwa Neno la Mungu, kukuza uhusiano wa karibu kabisa naye. Kuna vikwazo vingi na vitu vinavyohitaji wakati wetu. Lakini kwa uongozi wa Mungu, tunaweza kuondoa vitu vitakavyotuzuia. Kazia lengo lako macho na ujifunze kusema “hapana” kwa vitu ambavyo vinakukwaza na kukufanya usiweze kutimiza uwezo wake mkamilifu.


Dhamiria kuwa hakuna kitakachokuzuia kutimiza mpango wa Mungu na kusudi lake juu ya maisha yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon