Kuamini Ubora Wa Wengine

Kuamini Ubora Wa Wengine

Huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. 1 WAKORINTHO 13:7

Biblia inatufundisha kuamini ubora wa kila mtu kila wakati.

Hata hivyo, tukiacha tu mawazo yetu kutuongoza, mara nyingi huwa yanatuongoza katika fikra hasi. La kuhuzunisha ni kwamba, mwili usiongozwa na Roho Mtakatifu ni giza na hasi. Shukuru kuwa si lazima tutembee katika mwili, lakini tunaweza kuchagua kuongozwa na Roho (tazama Warumi 8:5). Tunapochagua kuruhusu Roho kutuongoza, tutaona ubora katika watu wengine, na tutajazwa na uhai na amani katika nafsi zetu.

Ninakuhimiza kuanza kuona watu wengine kama watoto wa Mungu badala ya maadui. Amua kupuuza udhaifu wao na uwaone vile Mungu anavyowaona. Shukuru kwamba Roho anaweza kukusaidia kuona ubora katika kila mtu kwenye maisha yako.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru leo, Baba, kwamba unasamehe dhambi zangu na hauzihesabu juu yangu. Ninaomba unipe nguvu zako ninapowafanyia wengine hivyo hivyo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon