Kuamua Kupenda

Chuma hunoa chuma; ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake. —MITHALI 27:17

Sisi wote tuna watu katika maisha yetu ambao wako kama karatasi ya kupiga msasa kwetu. Wengine wako kama kifurushi kizima cha karatasi za kupiga msasa. Amini usiamini, Mungu huwaweka katika maisha yetu kunoa makali yetu. Tuko kama almasi zilizo na makali. Tuna kitu kizuri na chenye thamani chini ya sehemu ngumu ya mwili wetu.

Mungu alipoanza kufanya kazi ya ukomavu wa kiroho ndani yangu, aliweka watu wengi katika maisha yangu ambao walikuwa wagumu sana kwangu mimi kushirikiana nao. Nikafikiri walihitaji kubadilika, lakini Mungu alitaka kuwatumia kunibadilisha. Lazima tujifunze kukabiliana na aina zote za watu na kufurahia vile wanavyotofautiana na sisi.

Dave anaweza kungoja kupata vitu kwa muda mrefu bila kusikitika, lakini mimi hutaka vitu kufanyika haraka. Yeye ni mtulivu na mimi huzungumza sana; anapenda kucheza muziki asubuhi na ninapenda kukiwa kutulivu. Nina hakika una watu maishani mwako ambao wako tofauti na wewe pia. Badala ya kukasirika, au kufikiria kwa kiburi kwamba wamekosea na wewe uko sawa, unafaa kuwakubali kwa upendo, vile tu Kristo anavyokutukubali sisi

Tunaweza kuamua kupendana na kuelewana miongoni mwetu bila kujali tulivyo au hali zetu zilivyo. Kwa sababu tunapowapenda tu watu wanaotuzunguka—hata wale wasiopendeka—tutajifungua kusoma kitu ambacho huenda Mungu anajaribu kutufundisha.


Chagua kutembea ndani ya upendo wa Kristo na umruhusu kukunoa kupitia kwa watu wengine anaoleta katika maisha yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon