Kuishi kwa Tumaini

Kuishi kwa Tumaini

Na tumaini hilo tunalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo. 2 WAKORINTHO 3:4

Mtu asiye na tumaini ni kama ndege iliyo katika barabara yake ikiwa na matangi yasiyokuwa na mafuta. Ndege ina uwezo wa kupuruka, lakini bila mafuta, haitaondoka kwenye barabara yake. Tumaini ndilo mafuta yetu—na ndiyo kwa sababu tumaini ambalo tunapata ndani ya Yesu ni kitu cha kushukuru kwacho.

Tumaini letu hutufanya tuanze na kumaliza kila changamoto tunayokabiliana nayo maishani. Bila tumaini, tutaishi kwa hofu na tutawahi kuhisi utimilifu. Tumaini hutuwezesha kukabiliana na maisha kwa ujasiri, uwazi na uaminifu. Linatuwezesha kuishi bila wasiwasi na kuhisi usalama. Hutuwezesha kuishi kihalisi.

Tunapojua sisi ni akina nani ndani ya Mungu, hatuna haja ya kujifanya sisi ni mtu tusiye kwa sababu tuko salama jinsi tulivyo—hata kama tuko tofauti na wale walio karibu nasi. Tumaini hutuwezesha kuishi maisha ya amani yaliyojaa furaha.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwa tumaini nililo nalo ndani yako. Asante kwamba sina haja ya kuishi maisha yasiyo yenye usalama, hofu na wasiwasi. Ninaweza kupaa katika hatma yangu kwa sababu unanipa nguvu ninazohitaji.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon