Kumngoja Mungu kwa Matarajio

Kumngoja Mungu kwa Matarajio

Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; kwa maana nitakuja kumsifu, aliye afya ya uso wangu, na Mungu wangu. —ZABURI 42:5

Iwapo ushawahi kuhisi kukata tamaa, hauko peke yako. Daudi alihisi vivyo hivyo pia. Lakini Daudi hakuruhusu kukata tamaa kumfadhaishe. Alipohisi hivyo, Daudi alimtumainia Mungu na kumngoja, akimsifu kama msaada wake na Mungu wake. Tunaweza kufanya vivyo hivyo tukichagua kufanya.

Ili kushinda hisia zake na hisi zilizomshusha, Daudi alidhamiria kumtazama Mungu, sio shida zake.

Daudi alijua kwamba iwapo angelenga kutazama kwenye upande mbaya wa mambo, ingekuwa rahisi kufadhaika na kukosa tumaini. Ndiyo kwa sababu alichagua kujihimiza na kujitia nguvu katika Bwana (1 Samweli 30:6) kila mara.

Tunapojipata katika hali inayokatisha tamaa, tunaweza kufuata mfano wa Daudi na kumngoja Bwana kwa matarajio, tukimsifu bila kujali vile hali zinazotuzunguka. Kadri tunavyomkaribia Mungu, ndivyo inakuwa rahisi kumfanya makazi yetu. Badala ya kukata tamaa na kufadhaika, tunaweza kuweka matumaini yetu ndani ya Bwana, na kumwamini kutukomboa.


Bwana hutufinika na kutulinda. Hutupigania vita vyetu tunapomsifu. (Mambo ya Nyakati 20:17, 20–21).

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon