Kuomba Maombi ya Ujasiri

Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. —YOHANA MTAKATIFU 16:24

Maombi yenye mafanikio kabisa ni maombi ya ujasiri. Hufanywa na waaminio walio na lengo maalum na wana ujasiri wa kuja mbele za Mungu na kuomba vitu wanavyohitaji maishani, bila aibu ya kufanya mahitaji yao yajulikane.

Kimojawapo cha vitu vikuu vinavyozuia watu kuomba kwa ujasiri ni kwamba wanatazama makosa yao badala ya kutazama yale mazuri ambayo Yesu amefanya. Biblia inatufundisha wazi kwamba Mungu “…alimfanya Yesu kuwa dhambi, yeye ambaye hakujua dhambi, ili ndani yake na kupitia kwake, tupate kuwa haki ya Mungu” (2 Wakorintho 5:21). Kwa sababu sisi ni wenye haki ndani yake, tunaweza kukikaribia kiti cha neema kwa ujasiri na mahitaji yetu (Waebrania 4:16).

Yohana 16:23–24 inatuambia tunaweza kuja kwa ujasiri mbele ya kiti cha enzi kwa jina la Yesu. Jina la Yesu lina nguvu. Tunapotumia jina la Yesu katika maombi yetu, sio fomula au hirizi tunayoweka mwishoni mwa kila kitu tunachoomba. Tunapoenda kwa jina la Yesu tunasema, “Baba, naja kwako kukuwasilishia Yesu alivyo—sio mimi nilivyo.”

Usikose uwazi au ukawa mwoga—kuwa jasiri! Utashangazwa na majibu utakayopokea.


Mungu anangoja kukushangaza na vitu vizuri—Je, uko tayari kuvipokea?

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon