Kupata Nafuu Kutokana na Uchungu

Kupata Nafuu Kutokana na Uchungu

Kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo—vazi la sifa badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito—wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe. Isaya 61:3

Kupata nafuu kutokana na uchungu au masikitiko ya aina yoyote sio tu kitu ambacho hufanyika kwa watu wengine na wengine kuepuka. Ni uamuzi! Unafanya uamuzi kusahau na kusonga mbele. Unajifunza kutokana na makosa yako. Unakusanya vipande vya maisha yako na kumpa Yesu, na atahakikisha kuwa hakuna kinachoharibiwa (tazama Yohana 6:12). Unakataa kutafakari kuhusu kile ulichopoteza; badala yake, unachukua hesabu ya vile vilivyobaki na kuanza kuvitumia kwa moyo wa shukrani.

Katika Kristo, huwezi tu kupata nafuu, lakini unaweza kutumiwa pia katika kusaidia watu wengine wapate nafuu. Kuwa mfano unaoishi wa mtu mwenye shukrani ambaye wakati wote hupata nafuu kutokana na matatizo hata kama ni magumu au hutokea mara kwa mara. Usiwahi kusema, “Siwezi tu kwenda.” Badala yake, sema, “Ninaweza kufanya ninachohitaji kufanya kupitia kwa Kristo. Sitakata tamaa, kwa sababu Mungu yuko upande wangu.”


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa kuwa unaleta uponyaji ndani ya moyo wangu na unaweza kunipa taji ya maua badala ya majivu. Ninaomba kwamba utanisaidia kuchuchumilia mbele, bila kukata tamaa. Ninataka kutumia tajriba zangu kusaidia wengine kupata huo uponyaji ambao nimepata.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon