Kupokea Himizo Lako

Kupokea Himizo Lako

. . .Kwa maana mimi nisipoondoka, huyo msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. —YOHANA 16:7

Je, wakati mwingine huwa unajipata ukitamani ungekuwa na himizo zaidi, labda kutoka kwa familia, marafiki au wafanya kazi wenzako? Ninafikiri huwa sote tunahisi hivyo wakati mmoja au mwingine. Unapohisi unahitaji himizo na watu wengine hawaonekani kukupa, unaweza kutia nguvu ndani ya Bwana (1 Samweli 30:6), na unaweza pia kupokea himizo kutoka kwa Roho wa Mungu.

Ulijua kwamba Roho Mtakatifu anaitwa “Mhimizaji”? Neno la kiGiriki la “Roho Mtakatifu” ni parakletos na hujumlisha faraja, kuinuliwa na himizo kama sehemu za ufafanuzi wake.

Yesu alituma Msaidizi, Mtia Nguvu, Mwiinuaji, na Mhimizaji alipotuma Roho Mtakatifu—na alimtuma kuwa katika ushirika wa karibu nasi. Anaisha ndani ya wale ambao ni waaminio ndani ya Yesu Kristo.

Iwapo unahitaji himizo, mtazamie Mungu kwanza. Hatawahi kukwambia kwamba hutaweza. Hatawahi kukwambia kwamba hakuna tumaini kwa kesi yako. Badala yake, atakuhimiza kwamba mambo yote yanawezekana ndani yake. Atakukumbusha kwamba anakupenda, yuko nawe, na anakupa nguvu unazohitaji kufanya yote aliyokuitia kufanya.


Fungua moyo wako kupokea faraja, hakikisho, na himizo kutoka kwa Roho Mtakatifu leo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon