Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. —Waefeso 6:12
Shetani hupigana dhidi yetu na mbinu yake moja ni kutufanya tuhisi vibaya kujihusu. Hutukumbusha kuhusu kutofaulu na udhaifu wetu wote, lakini tunahitaji kukumbuka kwamba Mungu anajua mambo yote kutuhusu na hata hivyo anatupenda.
Tunapigana vita vingi, lakini pengine vita vikuu tunavyopigana ni vile tunavyopigana nasi wenyewe. Huenda tukang’ang’ana na hisia kwamba tungefikia mengi maishani kuliko yale tuliyo nayo; huenda tukahisi kwamba tumekosa kufaulu kwa njia nyingi. Hatuwezi kubadilisha lolote kwa kusikitika na kung’ang’ana ndani yetu. Ni Mungu tu anayeweza kutubadilisha tunapomwamini. Atapigana vita vyetu na kushinda. Jukumu letu ni kuamini, kushirikiana naye, na kufuata uongozi wa Roho Mtakatifu.
Ni vigumu kufikia mahali ambapo tunaweza kujiambia ukweli kuhusu dhambi zetu na kutofaulu, kutoweza na makosa yetu ilhali huku tukijua kwamba tunaonekana kuwa hatuna maksoa mbele ya Mungu kwa sababu ya kile Yesu alifanya kwa niaba yetu alipotufia na kufufuka kutoka wafu. Iwapo una vita ndani yako, kujua kuwa wewe ni mwenye haki wa Mungu ndani ya Kristo ni ufunguo wenye uwezo mkuu wa kukuingiza katika amani na uwezo wa kiroho.
Tunaweza kubadilishwa tunapoabudu na kumtazama Mungu—sio tunapojitazama, tukijiongezea udhaifu wetu mwingi.