Kuwa Unayeweza Kutumika

Kuwa Unayeweza Kutumika

Basi ndugu zangu nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. —WARUMI 12:1

Iwapo wewe ni aaminiye, maisha yako yamewekwa wakfu kwa Mungu, na kutengwa kwa matumizi yake. Hujimiliki sasa; wewe ni sehemu ya kitu kikubwa sasa. Ni jambo la ajabu kufikiri kwamba maisha yetu sio yetu binafsi; tumenunuliwa kwa thamani (1 Wakorintho 6:20). Sisi ni wa Mungu na maisha yetu yana kusudi kubwa ndani yake!

Tunapomkaribia Mungu, tunagundua kwamba sisi ni wake, na kwamba sisi ni washirika pamoja naye katika maisha na tunafaa kujiandaa kwa matumizi yake ya kila siku.

Nilitumia miaka mingi nikiomba Mungu anipe nilichotaka. “Mungu, iwapo ungenipa hiki ama kile, basi nitafurahi.” Lakini Mungu akanionyesha furaha huja nikisalimisha mipango yangu kwake. Badala ya kumwomba kufanya nilichotaka, nilianza kumwuliza alichotaka kwa ajili ya maisha yangu.

Mungu hutaka tu tupatikane na tutumike. Tunaweza kufanya hivyo sisi sote! Tunaweza kusalimisha maisha yetu kwa Mungu, tukimwamini kufanya mpango wake mwema kwa ajili ya mustakabali wetu.


Huenda tusipate kila kitu tunachotaka. Lakini iwapo tutamwamini Mungu, tutatambua kwamba kile anachotaka kwa ajili ya maisha yetu ni kikuu kuliko kitu kingine chochote tunachoweza kufikiria.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon