Mabadiliko ni Mchakato

Mabadiliko ni Mchakato

Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi. —WAEBRANIA 6:15

Mabadiliko hayaji kwa urahisi. Sitawahi kusahau kuhusu mwanamke aliyenikabili siku moja baada ya kumaliza kufundisha. Kwa ghadhabu, aliweka mikono kiunoni na kuniambia, “nirudishie pesa zangu!” Nilishangazwa kiasi na taarifa yake, na nikajibu, “unamaanisha nini kwa kusema urudishiwe pesa?” Akasema “Joyce, nilikuwa ninatoa katika huduma yako, nanimekuwa nikifanya haya mambo unayosema tufanye na kwa muda wa wiki mbili nzima sasa, hakuna kilichobadilika!”

Lilikuwa jambo la kuchekesha kiasi lakini papo hapo, nilimweleza kwamba, sivyo inavyofanya kazi. Mabadiliko huchukua muda. Na subira huhitajika ili ifanye kazi kwa ufanisi kupitia kwa mchakato utakaoleta matokeo unayotaka. Aliondoka akiwa ameudhika kwa kuwa alitaka suluhu ya moja kwa moja na Mungu hafanyi hivyo. Ulipookoka, ulikanyaga barabara ilikuongoza kwenye safari ya mabadiliko katika maisha. Na maisha yetu yanabadilishwa kupitia kwa Neno la Mungu (Yakobo 1:21-25).

Ili kuishi katika ushirika wa karibu na wa ndani na Mungu, fanya uamuzi wa kuwa mfuasi na mwanafunzi katika maisha yako yote. Soma Neno. Sikiliza mafundisho kuhusu Neno. Hakuna kitu kizuri kuliko kuingiza Neno la Mungu katika moyo wako…ndiyo sehemu muhimu kabisa ya mchakato huo.


Biblia inasema tunarithi ahadi za Bwana kupitia kwa imani na uvumilivu (Waebrania 6:12), na imani huja kwa kusikia Neno la Mungu (Warumi 10:17).

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon