Yesu Aliishi Maisha ya Kutoa Shukrani

Yesu Aliishi Maisha ya Kutoa Shukrani

Na kumshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo. WAEFESO 5:20

Sehemu mojawapo ya nguvu za maombi ni nguvu za shukrani…kwa sababu hakuna maisha ya nguvu kando na maisha ya kutoa shukrani. Wakati wa huduma yake duniani, Yesu aliishi maisha ya shukrani. Alimpa Baba shukrani wakati mwingi na kwa vitu vingi.

Kwa mfano, alitoa shukrani kwa Mungu alipoimega mikate na samaki na kuwapa makutano (tazama Matayo 15:36). Alimshukuru Mungu kwamba alikuwa amesikia maombi yake kuhusu kumfufua Lazaro kutoka kwenye wafu (Yohana 11:41–42). Na alimpa Mungu shukrani alipowapa wanafunzi wake mkate na divai wakati wa mlo wao wa mwisho pamoja hata ingawa alijua mateso na kifo chake vilikuwa vimekaribia sana (tazama Marko 14: 22–23).

Iwapo ilikuwa muhimu kwa Yesu kuishi maisha ya kutoa shukrani, kwa hakika inafaa kuwa muhimu kwetu kufanya hivyo hivyo.


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwa mfano wa Yesu na kielelezo cha maisha ya shukrani ambacho alituonyesha. Nisaidie kuingia malangoni mwako kwa shukrani kila wakati ninapokuja kwako katika maombi. Wewe ni mwema na unastahili shukrani na sifa zangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon