Maombi Huzalisha Amani

Maombi huzalisha Amani

Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu zijulikane na Mungu. —WAFILIPI 4:6–7

Katika kifungu hiki, Mtume Paulo hasemi, “Omba na ufadhaike.” Badala yake, anasema “Omba na usifadhaike.” Kwa nini tuombe na tusifadhaike? Kwa sababu maombi ni njia muhimu ya kumtwika Bwana fadhaa zetu. Maombi ndiyo hufungua mlango wa Mungu kufanya kazi katika maisha yetu na maisha ya watu wengine.

Shetani anapojaribu kutupatia kitu cha kutufadhaisha, tunaweza kugeuka na kumpa Mungu fadhaa hiyo. Tukiomba kuhusu kitu halafu tuendelee kufadhaika kukihusu, tunachanganya chanya na hasi. Haya mawili hubatilishana na kuturudisha pale tulipoanzia—hatua ya sifuri.

Maombi ni nguvu chanya; fadhaa ni nguvu hasi. Mungu amenionyesha kuwa sababu inayofanya watu wengi waendeshe maisha yao kwa nguvu za chini kabisa kiroho ni kwamba wanabatilisha nguvu za maombi yao chanya kwa kuyapa nguvu hasi za fadhaa.

Mradi tu tunaendelea kufadhaika, hatumwamini Mungu. Ni kwa kuamini tu, na kuwa na imani na uhakika katika Bwana ndipo tunaweza kuingia rahani mwake na kufurahia amani ambayo inapita ufahamu wote.


Unaweza sasa kuamua kumtwika Bwana fadhaa zako zote na kuanza kuamini atakutunza.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon