Matendo dhidi ya Neema

Matendo dhidi ya Neema

Hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. —WAEFESO 2:5

Huwa tunasikitika kila mara kwa sababu tunajaribu kuishi kwa kazi zetu, ilhali maisha yetu yaliumbwa na kupangwa na Mungu ili tuishi kwa neema. Kadri tunavyojaribu kufikiria kile tutakachofanya ili tutatue utata wetu, ndivyo tunavyozidi kuchanganyikiwa, kufadhaika na kusikitika.

Unapofikia hali ya kusikitika, simama tu na useme, “Bwana, nipe neema (nguvu na uwezo wako).” Halafu uamini kwamba Mungu amesikia maombi yako, anayajibu na kufanya jambo katika hali hiyo.

Imani ndiyo njia ambayo mimi na wewe hupokea neema ya Mungu. Tukijaribu kufanya vitu peke yetu, bila kufunguka ili kupokea neema ya Mungu, basi hata tufikiri tuna imani kiasi gani, bado hatutapokea tunachomuomba Mungu.

Tunaweza kutumainia na kutegemea neema ya Mungu. Yuko karibu nasi, anajua tunachokabiliana nacho katika kila hali ya maisha, na atafanya mambo yawe mema tukimwamini ya kutosha kumruhusu kufanya hivyo.


Kumbuka, si kwa uwezo wala nguvu, lakini kwa Roho ambapo tunashinda vita juu ya adui yetu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon