Matendo ya Miujiza

Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima na mwingine neno la maarifa apendavyo Roho yeye yule; mwingine imani katika Roho … na mwingine matendo ya miujiza (1 WAKORINTHO 12:8-10)

Yesu alitenda miujiza mingi. Kwa mfano, aligeuza maji yakawa divai (soma 2:1-10) na kuulisha mkutano mkubwa kwa chamchana cha mvulana mdogo hata pakawa vikapu vilivyojaa mabaki (soma Yohana 6:1-13). Kuna aina nyingi za miujiza – miujiza ya kutoa, miujiza ya uponyaji, na miujiza ya ukombozi na kadhalika.

Mimi na Dave tumeona miujiza mingi kwa kipindi cha muda mrefu. Bila shaka tumeona miujiza ya uponyaji wa mwili na ukombozi kutokana na utumwa wa muda mrefu. Tumekuwa na tajriba ya miujiza ya utoaji- nyakati ambazo Mungu ametoa kwa ajili yetu binafsi na huduma kimiujiza kiasi cha kujua kwamba ni Mungu mwenyewe aliyeingilia kati katika hali yetu na kutupatia tulichohitaji.

Miujiza ni vitu visivyoweza kuelezwa, vitu amabvyo havifanyiki kwa njia za kawaida. Sisi wote tunaweza na tunafaa kumwamini Mungu kwa sababu ya miujiza katika maisha yetu. Usiridhike kuishi maisha ya kawaida huku karama ya miujiza ikiwepo. Mwombe na utarajie Mungu kutenda miujiza katika maisha yako na maisha ya watu wengine. Huyo huyo Mungu mmoja aliyegawanya Bahari ya Shamu anataka kukusaidia leo.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Usiridhike na vitu vya kawaida, tarajia visivyo vya kawaida.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon