Msamaha dhidi ya Hisi

Ukae kimya mbele za Bwana, nawe umngojee kwa subira; usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia zake, wala mtu afanyaye hila. — ZABURI 37:7– 8

Pengine uelewa mbaya kuhusu msamaha ni wazo kwamba iwapo hisia za mtu hazijabadilika, hajasamehe. Watu wengi wana hili wazo potofu. Wanaamua kusamehe mtu aliyewadhuru, lakini wakiendelea kuwa na hisia za hasira na kudhurika, wanahisi kwamba hawajamsamehe huyo mtu kikamilifu.

Unaweza kumtii Bwana na kufanya maamuzi timamu ya kiBiblia na uendelee kutohisi tofauti yoyote kwa muda mrefu tangu uamue kusamehe. Hapa ndipo imani inaweza kukupitisha. Umefanya kazi yako na sasa unamngoja Mungu kufanya kazi yake. Kazi yake ni kuponya hisia zako, kukufanya uhisi uponyaji wala sio kudhurika. Una uwezo wa kufanya maamuzi ya kusamehe, lakini ni Mungu pekee aliye na uwezo wa kubadilisha hisia zako juu ya mtu aliyekudhuru.

Uponyaji huchukua muda. Kwa hivyo usikose subira na kukata tamaa kama “hutahisi” kila kitu kikiwa sawa mara moja. Mungu yuko usukani, na anafanya kazi ya ajabu ndani yako na katika maisha yako.


Fanya uamuzi wa kumtiii Mungu, na umtumainie kubadilisha moyo wako. Hatimaye, hisia zako zitafuata na kuandamana na uamuzi wako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon