Mtihani wa Mtumishi

Kila mmoja kwa kadri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu. —1 PETRO 4:10

Kadri tunavyomkaribia Mungu, ndivyo anatupatia “nafasi” za kuwatumikia wengine kwa sababu hivyo ndivyo tunavyohitaji kuona kutumikia wengine. Tunapowatumikia wengine kila wakati, hawabarikiwi tu bali huleta furaha kuu kwenye maisha yetu. Yesu alitupatia mfano wa kuwa mtumishi kwa kuosha miguu ya wanafunzi na akisema, “..ili kama mimi nilivyowatendea (kwa zamu yenu), nanyi mtende vivyo” (Yohana 13:15).

Watu wengine hukosa kuishi kama watumishi kwa sababu hawajui wao ni akina nani ndani ya Yesu. Wanahisi kulazimika kufanya kitu ambacho wanaweza kufikiria ni “muhimu” ili kujiridhisha. Wanakosa kuelewa kwamba utambulisho wao huja kutokana na kile walicho ndani ya Kristo, sio vile umaarufu wa kazi zao ulivyo au nafasi zao. Ukiwa salama katika nafasi yako ndani ya Kristo, na unapopata nguvu na ujasiri wako ndani ya Mungu, unapata furaha kuu kwa kuwasaidia wengine unapopata kila nafasi ya kufanya hivyo.

“Mtihani wa mtumishi” ni vile tu tunakabiliana na nafasi ambazo Mungu anatupatia kuwa baraka kwa wengine. Mungu ametubariki na kutufanya kuwa baraka! Baraka za Mungu hazikusudiwi kutumiwa kwetu sisi peke yetu, lakini wakati wote kuwagawia walio karibu nasi.


Tafuta njia za kuwahudumia wengine leo, wakiwemo wale wa nyumbani mwako. Hii itakuwa tajriba kuu kwako na kwao.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon