Mungu Hubariki Utiifu

Mungu Hubariki Utiifu

Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kwelikweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu ; maana dunia yote pia ni mali yangu. —Kutoka 19:5

Neema ya Mungu na nguvu zipo kwa ajili yetu kutumia. Mungu hutuwezesha au kutupatia upako wa Roho Mtakatifu kufanya analotuambia tufanye. Wakati mwingine akishatuchochea kwenda upande mwingine, bado huwa tunajaribu kukazana kushikilia mpango wetu wa awali. Iwapo tunafanya kitu ambacho hajakikubali, huwa hashurutishwi kutupatia nguvu za kukifanya. Tunakifanya kwa nguvu zetu badala ya chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Kisha tunasikitika, kufadhaika, na kuchoka au kukosa kujidhibiti, kwa kupuuza vichocheo vya Roho.

Watu wengi wamefadhaika na kuchoshwa kutokana na kwenenda katika njia yao badala ya ile ya Mungu. Wanaishia kuwa katika hali za kufadhaisha wanapoenda upande tofauti na ule ambao Mungu aliwachochea kwenda. Kisha wanachoka katikati ya kutotii huko na kuishia kung’ang’ana ili kumaliza walichokianza nje ya njia ya Mungu, wakati huo wote wakimrai Mungu kuwabariki.

Tunashukuru, Mungu ni mwenye huruma, na hutusaidia katikati ya makosa yetu. Lakini hatatupatia nguvu na nishati ili tukose kumtii. Tunaweza kujiepusha na hali nyingi za kufadhaisha kwa kutii tu vichocheo vya Roho Mtakatifu kila wakati.


Utiifu zaidi kila mara ni sawa na mfadhaiko uliopungua!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon