Mwamba wa Msingi Thabiti

Mwamba wa Msingi Thabiti

Akawaambia nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? Simoni Petro akajibu akasema, wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.—MATHAYO 16:15–16

Petro aliposema kuwa Yesu ndiye alikuwa Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai, ilikuwa taarifa ya imani. Katika kutamka taarifa hii, Petro alikuwa akidhihirisha imani yake.

Sidhani Petro alitoa taarifa hiyo kikawaida. Ninafikiri alifanya hivyo na hakikisho na thibitisho ambalo lilimpendeza Yesu kwa sababu punde alimgeukia Petro na kumwambia kwamba amebarikiwa. Kisha akaendelea kusema kwamba ni juu ya mwamba huo wenye msingi thabiti wa imani ambapo angejenga kanisa lake.

Yesu alikuwa akimwambia Petro, “ukishikilia imani hii, itakuwa kitu cha mfano wa mwamba katika maisha yako, ambapo juu yake, nitaweza kujenga ufalme wangu ndani yako na kupitia kwako. Imani yako itajengwa hadi mahali ambapo hata milango ya kuzimu haitakushinda.”

Katika maisha yangu, mara nyingi nimepata kukata tamaa na kukosa kujua la kufanya, au kuhisi kwamba hakuna linalofanya kazi na kwamba kila mtu hakunitaka. Maneno ambayo nimesikia yakirudiwarudiwa, “Amini tu.”

Hii ahadi haikuwa ya Petro pekee yake. Yesu anatuambia maneno hayo hayo mimi na wewe. Amini tu!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon