Neema dhidi ya Matendo

Neema dhidi ya Matendo

Siibatili neema ya Mungu; maana ikiwa haki hupatikana kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa bure. —WAGALATIA 2:21

Ni jambo zuri kuja kwa Mungu kupitia kwa Yesu jinsi tu tulivyo, kwa kutegemea sio chochote bali damu ya Yesu kutusafisha dhambi zetu. Mioyo yetu imejaa shukrani kwa sababu tunajua hatustahili. Lakini kuanzia wakati huo kuendelea, kwa sababu moja au nyingine, huwa tunaelekea kutaka kuchuma vitu vingine vyote anavyotupatia.

Tunachukulia kwamba Mungu hatatubariki kwa kuwa tunafikiri kwamba hatustahili. Hatukusoma Biblia vya kutosha, hatukuomba vya kutosha, au tukakasirika tukiwa katika msongamano wa magari. Tunatafuta njia milioni moja za kufanya tusistahili upendo wa Mungu. Mungu hakomi kutupenda, lakini huwa tunakoma kuupokea.

Hata kama tunapoweka msisitizo kwenye imani, huwa tunajaribu kuishi maisha yaliyoletwa na Mungu na kupangwa na Mungu ili yaishwi kwa neema katika nguvu zetu, kwa kazi zetu. Si ajabu huwa tunafadhaika na kuchanganyikiwa—zote ni ishara kwamba tuko nje ya neema na ndani ya kazi.

Unapokuwa na tatizo katika maisha yako ambalo hujui vile utakavyokabiliana nalo, unachohitaji sio kufikiria na kuwaza zaidi kulihusu, lakini neema zaidi. Iwapo huwezi kupata suluhu ya tatizo lako, mtumainie Bwana akufunulie. Huna lazima ya kuchuma usaidizi wa Mungu au kuhitimu ili uupate—Anataka akuandae na kukuwezesha kila siku kupitia kwa neema yake…


Mahali kazi hushindwa, neema hushinda.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon