Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu, ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. YOHANA 16:24
Mara nyingi huwa nawaambia watu kuwa, jambo mojawapo ambalo wanafaa kufanya ili kufurahia maisha yao ni kurahisisha maisha yao—hilo linajumlisha maisha yao ya maombi pia. Sasa nikisema “rahisisha” maisha yako ya maombi, simaanishi kwamba usiombe kila wakati. Biblia inasema, “Omba bila kukoma” (1 Wathesalonike 5:17 Biblia). Tunaweza na tunafaa kwenda kwa Mungu kila mara katika maombi.
Ninachomaanisha ni kuwa ukijaribu kuwa na ufasaha sana, unaweza kutatiza maisha yako ya maombi sana hata yakafikia kiwango cha kutokuvumilia. Ni vizuri kujua kuwa hatuhitajiki kumpendeza Mungu kwa maombi yetu. Shukuru kuwa tunaweza kuongea tu naye kama rafiki; na kumwambia kwa kweli vile tunafikiri na kuhisi. Ukiwa na Mungu, unaweza kuwa mkweli kila wakati, na unaweza kuwa wewe binafsi kila wakati. Hauhitajiki kuwa na kiburi cha udini. Unaweza kuwa mkweli kwa Mungu na kutenga wakati kuwa naye.
Sala ya Shukrani
Baba, ninakushukuru kwamba kuongea nawe sio utaratibu mgumu. Ninashukuru kwanza ninaweza kuwa mimi nikiwa nawe na kuomba tu kilicho katika moyo wangu. Nisaidie kukumbuka kwamba maombi ni mazungumzo na kwamba ninaweza kuja kwako wakati wowote mchana kutwa.